Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maimu, wenzake kuanza kujitetea Desemba 14

Maimu Na Wenzanke Mhkmn (600 X 379) Maimu, wenzake kuanza kujitetea Desemba 14

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kusikiliza utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na wenzake wanne Desemba 14 na 15, 2021.

Mbali na Maimu wengine ni aliyekuwa Ofisa Usafirishaji Nida George Ntalima, Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo ,aliyekuwa Meneja Biashara wa Nida, Aveln Momburi na Mkurugenzi wa Sheria, Sajina Raymond wanakabiliwa na mashtaka 45 likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.

Wakili wa Serikali, Kija Lizingana leo Jumatano Novemba 17, 2021 amesema shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa hivyo ameiomba mahakama hiyo ipange kwaajili ya washtakiwa hao kuanza kujitetea.

"Kesi ilikuja kwaajili ya kutajwa naiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza utetezi," aliomba Lizingana

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu ameahirisha hadi Desemba 14 na 15, 2021 Kwa ajili ya utetezi.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, matumizi mabaya ya madaraka na kutumia nyaraka kumdanganya muajiri

Chanzo: mwananchidigital