Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maimu augua, Kesi yashindwa kuendelea

Maimu Nida Dickson Maimu anakabiliwa na mashtaka 45

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa( NIDA) Diskson Maimu, kuumwa.

Maimu na wenzake wanne, wanakabiliwa na mashtaka 45 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 1.175 bilioni.

Leo Jumanne Mei 10, 2022 shauri hilo liliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya Maimu kuanza kujitetea baada ya mahakama hiyo kumkuta na kesi ya kujibu, yeye na wenzake wanne.

Mahakama hiyo iliwakuta na kesi ya kujibu washtakiwa wote Agosti 11, 2021, baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 26 na vielelezo 45 vilivyotolewa na upande wa mashtaka, wakati wa usikilizwa wa shauri hilo.

Hata hivyo, leo shahidi huyo alipopanda kizimbani, aliieleza mahakama hiyo kuwa anaumwa na hivyo aliomba kesi hiyo iahirishwa hadi kesho ili aweze kwenda hospitali kupatiwa matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live