Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yawakuta na hatia wafanyakazi wanne wa Veta

Hukumu Pc Data Mahakama yawakuta na hatia wafanyakazi wanne wa Veta

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu waliokuwa wafanyakazi wanne wa Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) wakikabiliwa na shtaka la kutumia madaraka yao vibaya.

Washtakiwa hao ni Peter Sinzya, Jesse Bachumba, Gerard Laswai na Yasinta Mwakileo.

Uamuzi huo umetolewa jana Jumatatu Aprili 17, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo washtakiwa hao wanakesi ya kujibu au laa.

Mrio alisema mahakama imewakuta washtakiwa hao na kesi ya kujibu baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake kwa kuwaita mahakamani mashahidi tisa huku ikitoa vielelezo 17.

Kwa upande wa Jamhuri ikiwakilishwa na wakili Mwandamizi, Thuwaiba Hussein huku Upande wa utetezi ukiwakilishwa na Nickson Tugala, Godfrey Kizito, Prisca Mchimbi na Afrika Mazoea.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu, Mrio aliahirisha kesi hiyo huku akisema ushahidi wa upande wa utetezi utaanza kusikilizwa Mei 8, 2023.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa washtakiwa hao kwa pamoja wakiwa wafanyakazi walitumia madaraka yao vibaya kwa kumshauri Mkurugenzi Mkuu wa Veta kutoa zabuni ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Geita kwa Kampuni ya Skyward huku ikiwa haina uwezo wa kutekeleza mradi huo.

Inadaiwa kati ya mwaka 2015 na mwaka 2018 washtakiwa hao wakiwa wajumbe wa kamati waliandaa ripoti ya upembembuzi akinifu ambayo ilimshauri mkurugenzi kutoa tenda hiyo ya ujenzi wa chuo cha Veta kilichopo Geita wakati wakijua mkandarasi huyo alikuwa hana uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Chanzo: mwanachidigital