Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yawajia juu ma-RC, DC ukamataji watu hovyo

MAHAKAMA WEB Moja ya jengo la Mahakama Kuu, Mkoani Tanga

Fri, 11 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya nchini wameshauriwa kutotumia vibaya sheria ya kuweka watu ndani saa 48, na badala yake wafuate taratibu pindi wanapotaka kutumia sheria hiyo.

Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na Kaimu Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Dkt. Gerald Ndaki alipokua akizungumza na Waandishi wa habari.

Amesema ni vizuri kila kiongozi akatambua mipaka ya majukumu yake, huku akiheshimu utu na mamlaka yake pasipo kuvunja taratibu za utumishi.

Aidha amesisitiza suala la usimamizi wa haki na amani katika maeneo yote nchini kupitia Wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama ngazi za mikoa na wilaya. Mara kadhaa wanaharakati wamekua wakikemea matumizi ya sheria hiyo ambayo inawapa mamlaka makubwa wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwasweka watu rumande kwa saa 48.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live