Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yawahukumu watu watatu miaka 25 kila mmoja

Fri, 21 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Watu watatu wamehukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka 25 jela kwa kukutwa na meno sita ya Tembo na silaha moja aina ya Smg.

Akitoa hukumu hiyo leo Ijumaa Desemba 21, 2018 Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti Ismael Ngaile amesema ushahidi uliotolewa hukuacha shaka.

Amesema Mwita Joseph (36) mkazi wa Loretto Serengeti, Amos I Luhazi (45) wa Usinge Tabora na Jackson Makuru (43) mkazi wa Bunyambo Kigoma kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 25 jela.

Mapema Mwendesha mashitaka wa Serikali, Emmanuel Zimbabwe amesema washitakiwa walikamatwa Oktoba 2016 katika eneo la Merenga ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Walifikishwa mahakamani kwa makosa manne ya uhujumu uchumi katika kesi namba 60/2016.

Amesema siku hiyohiyo washitakiwa hao walikutwa na bunduki aina ya Smg Kimyume cha sheria.



Chanzo: mwananchi.co.tz