Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yawabana wasimamizi wa Mirathi ya Mengi

Mengi Mirathi Marehemu Reginald Mengi enzi za Uhai wake akiwa na mkewe

Fri, 15 Apr 2022 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Watoto Kisutu imewabana wasimamizi wa mirathi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, kwa kukataa kuwahudumia watoto wake wadogo aliowazaa na mjane wake, Jacqueline Ntuyabaliwe.

Mahakama hiyo imetoa msimamo huo katika uamuzi wake wa pingamizi lililowekwa na wasimamizi hao wa mirathi hiyo, Abdiel Mengi (mtoto wa marehemu wa mke wa awali) na Benjamin Mengi (mdogo wa marehemu Mengi), dhidi ya shauri la matunzo ya watoto.

Mahakama katika uamuzi wake juzi, ilikubaliana na hoja za wakili wa wadai na ikazikataa hoja zote za pingamizi la wadaiwa, hivyo ikatupilia mbali pingamizi hilo.

Shauri hilo la madai namba 50 la mwaka 2022, limefunguliwa na mjane Jacqueline, kama mlezi wa watoto hao akidai matunzo ya watoto hao ikiwamo ada ya shule, baada ya wasimamizi hao wa mirathi kukataa kutoa huduma kwa watoto hao, akiiomba Mahakama hiyo iwalazimishe kuwahudumia.

Walidai maombi hayo yamefunguliwa dhidi ya watu wasiostahili, badala yake hilo ni jukumu la wazazi.

Jacqueline anadai kuwa watoto hao walikuwa wakigharamiwa na baba yao wakati wa uhai wake ada ya shule pamoja huduma nyingine zote walizostahili kutokana na kipato alichokuwa anakipata.

Hata hivyo, wadaiwa kupitia kwa mawakili wao, Nakazael Tenga, Hamis Mfinanga na Grayson Laizer waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isilisikilize shauri hilo.

Chanzo: Mwananchi