Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yatupilia mbali ombi la kina Sabaya

SABAYA YANGA MAHAKAMANI Mahakama yatupilia mbali ombi la kina Sabaya

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro ametupilia mbali ombi la upande wa utetezi walilolitoa Agusti 12, 2022 wakiomba mahakama hiyo iwaachie huru, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne na upelelezi uendelee wakiwa huru.

Ombi hilo limetupiliwa mbali leo Jumatatu, Agosti 29, 2022 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Salome Mshasha akisema kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka wala kibali cha kusikiliza kesi hiyo, haiwezi kutoa uamuzi yoyote wala kuamuru upande wa mashtaka kuharakisha kesi hiyo na hivyo kutupilia mbali ombi hilo.

Amesema pamoja na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, ni vyema upande wa mashtaka wakawa makini kwani mahakama ni chombo cha kutenda haki na wananchi huko nje wanataka kuona hiyo haki ikipatikana.

Awali, Wakili wa utetezi, Hellen Mahuna ameomba upande wa utetezi kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo, ili washtakiwa waweze kupata haki zao kwa kuwa wako magereza na wanateseka.

"Kuanzia Juni 1, 2022, kesi hii ilipokuja kwa mara ya kwanza, upande wa Jamhuri ulisema upelekezi umekamilika, ombi letu upande wa nashtaka utilie mkazo kile walichokisema kwa kuwa washtakiwa wako magereza na wanateseka," amesema

Naye Wakili upande wa mashtaka, Sabitina Mcharo amepokea ombi hilo la upande wa utetezi la kuharakisha kesi hiyo na kusema upelelezi utakamilika. Advertisement

Kesi hiyo inayomkabili Sabaya na wenzake wanne imeahirishwa tena hadi Septemba 11, 2022, huku sababu zikitajwa ni kutokamilika kwa upelelezi wa shauri hilo.

Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka saba likiwamo kosa la uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu, pamoja na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Juni 1, 2022, Sabaya na wenzake wanne walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kusomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live