Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yatupa pingamizi kesi ya shehena ya dhahabu

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na upande wa utetezi kupinga kielezo PH3 ambayo ni gari iliyokamatwa ikiwa na shehena ya dhahabu isitolewe mahakamani hapo na shahidi wa kwanza.

Uamuzi huo mdogo katika kesi hiyo namba 1/2019 ya kusafirisha shehena ya dhahabu kilo 319 zenye thamani ya Sh27.18 bilioni na fedha taslimu Sh305 milioni, inayowakabili waliokuwa askari polisi wanane umetolewa leo Jumanne Mei 14, 2019 katika kesi hiyo.

Aprili 29 upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Steven Makwega uliweka pingamizi kwa shahidi wa kwanza Maxmilian Katabazi ambaye ni mlinzi katika kivuko cha Kigongo asitoe kielelezo hicho kwa madai tayari kilishatolewa kwa washtakiwa wanne ambao walikiri kosa wakalipa faini na kuachiwa huru.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rhoda Ngimilanga anayesikiliza shauri hilo amesema mahakama inalitupilia mbali pingamzi hilo kwa sababu ushahidi huo haumalizi kesi.

Hata hivyo upande wa utetezi ulikubaliana na uamuzi huo na kuendelea na shauri.

Kesi hiyo inawakabili aliyekuwa mkuu wa operesheni mkoa wa Mwanza, Morice Okinda, E. 6948 D/CPL. Kasala, F. 1331 PL. Matete, G. 6885 D/C Alex na G. 5080 D/C Maingu.

Pia Soma

Wengine ni G. 7244 D/C Timothy, G. 1876 D/C Japhet, H. 4060 D/C David Kadama ambao walifikishwa mahakamni hapo kwa mara ya kwanza Januari 11 mwaka huu.

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na makosa matano ya kutakatisha fedha, uhujumu uchumi na kula njama za kupanga uhalifu, makosa wanayodaiwa kuyatenda kati ya Januari 4 na 5 mwaka huu.

Waliokwepa kifungo ni wafanyabiashara Hassan Sadiq ambaye alikuwa mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Emmanuel Mtemi, Kisabo Nkinda na Sajid Hassan.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz