Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yatupa pingamizi kesi kina Sabaya

Sabaya Ngoma Ngumu Mahakama yatupa pingamizi kesi kina Sabaya

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya rufaa iliyofunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watano.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Desemba 14, 2022 na Jaji Salma Maghimbi ambaye anasikiliza shauri hilo, baada ya jana kusikiliza hoja za pande zote mbili.

Jana mawakili wa Sabaya na wenzake watano wameweka pingamizi la awali katika kesi ya rufaa waliyofunguliwa na Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live