Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yatoa hati kumkamata anayegushi nyara za serikali

Nyara Serikali Mahakama yatoa hati ya kumkamata anayedaiwa kugushi nyara za serikali

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata, mshtakiwa Ashrafu Maumba (37), baada kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa.

Pia mahakama hiyo imetoa hati kwa wadhamini wa mshtakiwa huyo kufika mahakamani hapo kujieleza sababu ya wao kushindwa kumfikisha mshtakiwa mahakamani Maumba ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya jinai namba 271/2016, ameshindwa kufika mahakamani hapo leo Alhamisi Septemba, wakati shauri hilo lililpoitwa kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mshtakiwa huyo na wenzake wawili, wanakabiliwa na mashtaka 140 ya kughushi nyaraka mbalimbali za Serikali, vikiwemo vyeti vya kumaliza kidato cha nne, sita, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya vyuo mbalimbali, kadi na leseni za magari, vitabu vya stika za bima na mabunda mawili ya nembo zenye mng'ao zinazotumika katika vyeti vinavyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).

Pia wanadaiwa kukutwa na mihuri ya moto na isiyokuwa ya moto, nyaraka mbalimbali za TRA, risiti za malipo za Comesa na risiti za malipo za Shirika la Bima la Taifa (NIC) na nyaraka za bima ya Nico na Allience.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Septemba 9, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Joseph Luambano baada ya mshtakiwa kushindwa kufika mahakama kwa mara ya pili, kusikiliza kesi yake bila kutoa taarifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live