Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yataka upelelezi kesi ya vigogo Udart ukamilike haraka

46092 Pic+kisena Mahakama yataka upelelezi kesi ya vigogo Udart ukamilike haraka

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka umetakiwa kuhakikisha upelelezi unakamilika kwa wakati katika kesi inayowakabili Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart), Robert Kisena (46) na wenzake watatu .

Kisena na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 19 likiwemo la utakatishaji fedha na kuusababishia Mradi wa Udart hasara ya zaidi ya Sh2.41 bilioni.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na raia wa China, Cheni Shi (32).

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Pendo Temba kudai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amewataka upande wa mashtaka kuhakikisha shauri hilo wanalifuatilia ili upelelezi ukamilike kwa wakati.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 25 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.

Katika mashtaka yao yamo ya  kujenga kituo cha mafuta bila kibali, kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa pamoja na shtaka la wizi wakiwa wakurugenzi.

Pia wanakabiliwa na mashtaka manne ya utakatishaji fedha, kughushi manne, kutoa nyaraka za uongo manne, mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la kuusababishia mradi huo hasara.



Chanzo: mwananchi.co.tz