Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yataka aliyejifanya Waziri Mbarawa akamatwe

89182 Mahakama+pic Mahakama yataka aliyejifanya Waziri Mbarawa akamatwe

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata mfanyabiashara, Wilfred Massawe  baada ya kukiuka masharti ya dhamana kwa kushindwa kufika mahakamani.

Mbali na kutoa hati ya kumkamata, mahakama hiyo imetoa hati ya wito  kwa wadhamini wa mshtakiwa huyo kufika mahakamani kujieleza kwa nini hawakumpeleka Massawe mahakamani.

Massawe anakabiliwa na mashtaka  manne ikiwemo ya kujipatia Sh700,000 kwa njia ya udanganyifu na kujifanya Waziri wa Maji,  Profesa Mbarawa kosa alilolitenda wakati msomi huyo alipokuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Desemba 19, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

" Kutokana na mshtakiwa kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa, mahakama imetoa hati ya kumkamata  popote alipo, pia imetoa wito kwa wadhamini wafike mahakamani kujieleza sababu za wao kushindwa kumfikisha mshtakiwa mahakamani,” amesema Hakimu Ally.

Kabla ya kutolewa kwa hati hiyo, wakili wa Serikali, Janeth Magoho alidai kuwa upande wa mashtaka wanaye shahidi ambaye ni Profesa Mbarawa.

Chanzo: mwananchi.co.tz