Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yapokea video kesi ya kina Mbowe

68329 Pic+mbowe

Fri, 26 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kamera na mikanda miwili ya video ili itumike kama ushahidi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mbowe na viongozi wengine wanane wa chama hicho wakiwemo wabunge sita wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 112/2018 yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi wanayodaiwa kuyafanya Februari 16, 2018 wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.

Mahakama hiyo ilipokea vielelezo hivyo na kutupilia mbali pingamizi lililokuwa limewasilishwa na upande wa utetezi kwa madai havijakidhi vigezo vya kisheria.

Uamuzi huo wa kuvipokea vielelezo hivyo ulisomwa jana Alhamisi Julai 25, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Simba alisema ushahidi uliotolewa na shahidi wa sita katika kesi hiyo, ambaye ni askari polisi mwenye namba F 5392 Koplo Charles, unakidhi vigezo vyote vilivyopo katika kifungu 18 cha Sheria ya Miamala ya Kieletroniki.

Soma gazeti la Mwananchi la leo Ijumaa Julai 26, 2019 kwa habari zaidi.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz