Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yamuamuru mfanyabiashara aachie ardhi

8f74db9dac4f7f27be3482200551b07d.jpeg Mahakama yamuamuru mfanyabiashara aachie ardhi

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imemuamuru mfanyabiashara jijini Arusha, Philemon Mollel aondoke kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari saba alilowekeza kituo cha mafuta na biashara nyingine.

Kesi hiyo ya madai namba 1/2017 ilikuwa ikisikilizwa na Jaji Mosses Mzuna na aliridhika na ushahidi uliotolewa ambao umeonesha pasipo na shaka kwamba eneo hilo lililopo Nguleo, jiji Arusha, William Taitus Mollel ni mmiliki wake halali.

Uamuzi wa Jaji Mzuna wa Mei 11 mwaka huu amezingatia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili vikiwamo vielelezo vya umiliki vilivyothibitisha kuwa William ni mmiliki halali.

Kesi hiyo ilidumu kwa zaidi ya miaka mitano na jana ilishuhudiwa walinzi kutoka kampuni binafsi ya ulinzi wakivamia eneo la kituo hicho cha mafuta.

Walinzi hao walikuwa wakitaka kukishikilia kituo hicho lakini polisi wenye silaha za moto walifika kwenye eneo la tukio na kuwasambaratisha walipojaribu kuleta vurugu.

William aliishukuru Mahakama kwa kutenda haki uamuzi wale, ambapo Mollel alidai kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama na amekata rufaa.

Alidai mwaka 2009 alinunua eneo hilo lenye viwanja vinne kutoka kwa Jimmy Taitas Mollel kwa Sh milioni 95 kwa kila kiwanja ili awekeze kituo cha mafuta na sehemu ya kuoshea magari.

Alidai mwaka 2017 familia ya Taitas ilibadili msimamizi wa mirathi kwa kumteua mdogo wao William Taitas Mollel na mwaka 2017 alifungua shauri hilo mahakamani kudai eneo hilo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz