Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yamnyima dhamana Kiringo anayetuhumiwa kulawiti mtoto

3937 28467777 1005091786323729 4077350834286165061 N TZW

Mon, 5 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyopo Unguja (Vuga), Valestine Andrew Katema ametupilia mbali ombi la dhamana ya mshtakiwa wa kosa la kulawiti mtoto wa umri wa miaka 13, Hassan Aboud Talibu almaarufu Kiringo.



Kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2018 ya kosa la jinai iliyowasilishwa mahakamani hapo ilianza kusikilizwa jana na hakimu huyo amesema, ametupilia mbali ombi hilo kutokana na kosa lenyewe sambamba na sababu za maombi hayo kukosa nguvu.

Amesema, amefikia uamuzi huo kwa ajili ya kuhofia usalama wa mshtakiwa, kutokana na jamii kuchoshwa na vitendo hivyo vilivyokidhiri ambapo huenda wananchi wanaweza kujichukulia sheria mkononi.

Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 13, mwaka huu.

Chanzo: bongo5.com