Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yambana kigogo Chadema, yamwita kujieleza

52563 Pic+mahakama

Tue, 16 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemtaka Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema, Dk Vicent Mashinji kuieleza mahakama kwa nini ameshindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo mahakamani hapo.

Dk Mashinji ambaye ni mshtakiwa wa sita katika kesi ya kufanya mikusanyiko isiyo halali, inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho, ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa yupo kwenye kesi nyingine iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea mkoani Ruvuma.

Dk Mashinji ametakiwa kufika mahakamani hapo Aprili 17, 2019 (Jumatano) na kuieleza mahakama hiyo sababu za yeye kushindwa kufika mahakamani hapo, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Dk Mashinji na wenzake wanakabiliwa na makosa 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam waliku?a njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko la kutawanyika.

Kutokana na hilo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano Aprili 17, 2019.



Chanzo: mwananchi.co.tz