Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yakataa uchunguzi wa video kesi ya mauaji ya muuza madini

Mahakama Yakataa Uchunguzi Wa Video Kesi Ya Mauaji Ya Muuza Madini Mahakama yakataa uchunguzi wa video kesi ya mauaji ya muuza madini

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama imekataa kupokea hati ya uthibitisho wa uhalisia wa picha za video kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis, inayowakabili maofisa saba wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara.

Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hati hiyo imeandaliwa chini ya kifungu cha Sheria kisichohusika.

Jaji Edwin Kakolaki anayesikiliza kesi hiyo, amesema Kifungu Cha 202 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Ushahidi kilichotumika kuandaa hati hiyo inalenga kuthibitisha uhalisia wa picha za video hizo hakihusiki kwa kuwa kifungu hicho hakishughuliki na picha za video.

Hivyo, amesema kwa sababu hiyo hati hiyo haiwezi kuthibitisha video hizo na ameutupilia mbali.

Hata hivyo, mahakama hiyo ilikataa hoja nyingine za pingamizi la kupokea hati hiyo zilizoibuliwa na upande wa utetezi kupitia kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Majura Magafu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live