Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yakataa kupokea barua ya Chadema

87319 CHA Mahakama yakataa kupokea barua ya Chadema

Fri, 6 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa kupokea barua ya katibu mkuu wa  Chadema, Dk Vicent Mashinji aliyomwandikia msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Kinondoni kuhusu mawakala wa chama hicho kutopewa nyaraka za utambulisho na kiapo. Leo Alhamisi Desemba 5, 2019 mahakamani hapo  wakili wa utetezi, Peter Kibatala alimwonyesha Dk Mashinji barua iliyotoka kwa mkurugenzi wa uchaguzi, Ramadhan Kailima ikifafanua sheria na kanuni za uchaguzi na kumtaka aithibitishie mahakama kama anaitambua na aiombe ipokelewe kama sehemu ya kielelezo. Kabla ya mahakama kuhakiki na kupokea barua hiyo, wakili mwandamizi wa Serikali, Wankyo Simon aliomba mahakama hiyo kutopokea barua hizo kwa sababu zilionyesha kwenda kwa msimamizi wa Kinondoni, zikitokea ofisi  za Chadema na kusainiwa na Peter Msazye. Wakili wa Serikali mkuu, Faraja Nchimbi amedai hata kama Dk Mashinji ni mtunzaji  wa nyaraka hizo bado haitoshi mahakama hiyo kupokea vielelezo hivyo ambavyo ameshindwa kuiaminisha. Akitoa uamuzi  wa suala hilo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema kutokana na sababu za kisheria barua hizo haziwezi kupokelewa kwani hazionyeshi ni kwa njia gani zilimfikia mshtakiwa huyo. Amesema zilisainiwa na katibu wa wilaya,  Peter Msazye na kwamba shahidi huyo ameshindwa kutoa maelezo ya wazi kuhusu uhusiano wake na barua hizo. "Barua hizi haziwezi kupokelewa kisheria kwani hazikuonyesha kwa njia gani zilimfikia Dk Mashinji, zilisainiwa na katibu wa wilaya. Kutokana na sababu hizo mahakama haiwezi kupokea barua hizo kama sehemu ya ushahidi,” amesema Hakimu Simba. Dk Mashinji na viongozi wengine wanane wa chama hicho akiwemo mwenyekiti, Freeman Mbowe wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki. Wanadaiwa kushawiki hali ya kutoridhika, uchochezi wa makosa yanayodaiwa kutendeka kati ya Februari Mosi hadi 16, 2018 jijini Dar es Salaam. Wengine ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar); Esther Matiko (Tarime Mjini); John Heche (Tarime Vijijini), Ester Bulaya (Bunda); Halima Mdee (Kawe) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).

Chanzo: mwananchi.co.tz