Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaelezwa jalada waliokutwa na dawa za kulevya lipo kwa DPP

30003 DPP+PIC TanzaniaWeb

Tue, 4 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Jalada la kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili, Ayub Kiboko na mkewe, Pilly Mohamed  lipo ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kulipitia.

Wakili wa Serikali, Elia Athanas ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Desemba 3, 2018 wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Athanas amedai mbele ya hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, kuomba kupangiwa tarehe nyingine kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.

Baada ya kusikiliza maelezo hayo hakimu ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 17, 2018 kesi hiyo itakapotajwa tena.

Kiboko na mkewe wanakabiliwa na shtaka moja katika kesi ya uhujumu uchumi namba 29/2018, wakidaiwa kusafirisha dawa za ku?evya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 251.25.

Wanadaiwa Mei 23, 2018 eneo la Tegeta Nyuki Masaiti wilaya ya Kinondoni walisafirisha dawa hizo.

Washtakiwa hao wamerudishwa rumande  kutokana na shtaka linalowakabili kutokuwa na dhamana.



Chanzo: mwananchi.co.tz