Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaamru MC Luvanda kukamatwa

23601 Luvanda+pic TanzaniaWeb

Wed, 24 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeamuru mshereheshaji maarufu nchini Tanzania, Anthony Luvanda ‘MC Luvanda’ kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kusafiri kwenda nchini China bila ya ruhusa ya Mahakama.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ametoa hati ya kukamatwa kwa Luvanda, leo Jumanne Oktoba 23, 2018 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Kabla ya kutolewa kwa amri hiyo, Wakili wa Serikali Patrick Mwita amedai mahakamani hapo, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa lakini mshtakiwa hayupo mahakamani.

"Mshtakiwa akamatwe mara moja na kuletwa mahakamani ajieleze kwa nini asifutiwe dhamana yake kwa kukiuka masharti ya dhamana,” amesema Hakimu Shaidi.

Kesi imeahirishwa hadi Novemba 19, 2018, upelelezi bado haujakamilika.

MC Luvanda pamoja na kampuni yake, wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kutumia kikoa ambacho hakijasajiliwa Tanzania.

MC Luvanda anashtakiwa pia kwa kutoa  maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali cha Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mbali na MC Luvanda mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni kampuni ya Luvanda ya Home of Events Company Limited.

MC Luvanda  na kampuni anayomiliki ya Home of Events Company Ltd Limited  wanadaiwa kutumia kikoa ambacho hakijasajiliwa Tanzania.

Inadaiwa kati ya Februari 24 na Septemba 2018 katika jiji la Dar es Salaam,  mshtakiwa huyo alianzisha na kutumia mtandao wa  www.mcluvanda.com ambao haukuwa na kikoa cha .tz.

Pia, inadaiwa katika kipindi hicho mshtakiwa alianzisha na kutumia mtandao huo ambao haukuwa na kikoa cha .tz.

Aidha imedaiwa, mshtakiwa huyo alitoa huduma ya online bila ya kuwa na kibali.

MC Luvanda anadaiwa katika kipindi hicho  alitoa huduma hiyo kupitia online TV  ifahamikayo kama MC Luvanda pasipokuwa na kibali toka TCRA.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa Luvanda alikana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na kitambulisho ambaye alisaini bondi ya Sh 5 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz