Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaagiza maofisa ofisi ya DPP kwenda gereza la Keko

Mahakama yaagiza maofisa ofisi ya DPP kwenda gereza la Keko

Fri, 24 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeilekeza ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP) kwenda gereza la Keko kujua ukweli kuhusu washtakiwa wa kesi ya mauaji ya mwanaharakati  wa kupambana na ujangili, Wayne Lotter.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Januari 24, 2020 baada ya mshtakiwa Nduimano Zebadayo kudai mbele ya ya Hakimu mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa yeye pamoja na mwenzake, Habonimana Nyandwi hawapewi chakula maalumu wanachotakiwa kupewa raia wa kigeni waliopo mahabusu. Washtakiwa hao ni raia wa Burundi.

"Sijasema chakula kimesitishwa,  sisi tumeondolewa kwenye orodha ya kupewa chakula maalumu kwa ajili ya raia wa nje, tunapewa chakula na wenzetu Watanzania. Ninahoji kwa nini tuondolewe vyakula hivyo pamoja na kupewa  mahitaji mengine  ikiwemo sabuni, dawa ya meno na hatuna hata ndugu wa kutuletea hivyo vitu," amedai Zebedayo.

Awali, wakili Faraji Nguka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na taarifa aliyoipata kipindi cha nyuma raia wa nje waliokuwa gerezani walikuwa wanapewa vyakula maalumu, lakini kutokana na bajeti iliyopo wanapewa vyakula vya aina moja pamoja na mahabusu wa Tanzania.

Baada ya maelezo hayo hakimu Isaya amesema mahakama hiyo inaelekeza ofisi ya DPP kwenda  gerezani ili kujua shida inayowakabili

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 7, 2020.

Pia Soma

Advertisement
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya mauaji namba 9 ya mwaka 2017 ni Robert Mwaipyana, Godfrey Salamba, Inocent Kimaro, Chambie Ally  na aliyekuwa ofisa wa benki ya NBC, Robert Mwaipyana.

Wengine ni aliyekuwa meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi, Rahma Almas, Mohammed Maganga,  Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leornad Makoye, Amino Sham, Joseph Lukoa, Gaudence Matemu na Abuu Mkingie.

Katika kesi ya msingi washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya mauaji ya Lotter.

Katika shtaka la pili, wanadaiwa Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie iliyopo wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, wanadaiwa kumuua Lotter.

Chanzo: mwananchi.co.tz