Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaagiza Wema Sepetu akamatwe

62112 WEMAPIC

Wed, 12 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Juni 11, 2019  imetoka hati ya kumkamata mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu baada ya kukiuka masharti ya dhamana.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde baada ya mshtakiwa kushindwa kufika mahakama kusikiliza kesi inayomkabili.

Kabla ya kutoa uamuzi huo wakili wa Serikali,  Silyia Mitanto amedia kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi lakini Wema na mdhamini wake wote hawakuwepo mahakamani.

Baada ya kueleza hayo, Ruben Simwanza ambaye ni wakili wa Wema amesema mteja wake alikuwepo katika mahakama hiyo lakini aliugua tumbo na kulazimika kuondoka.

Baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, hakimu Kasonde amesema, “Kama amekuja mahakamani halafu akaondoka bila kutoa taarifa, mahakama itajuaje kama alikuja? Alishindwa nini kutoa taarifa mahakamani.”

Baada ya kueleza hayo hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 huku akitoa hati hiyo ya Wema kukamatwa.

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz