Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama kutoa uamuzi kesi ya mwanafunzi LST

Uamuzi Pic Lst Mahakama kutoa uamuzi kesi ya mwanafunzi LST

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Maombi ya mwanafunzi wa Shule ya Sheria kwa Vitendo Tanzania (LST), Alexander Barunguza kuhusu kesi yake ya Kikatiba inayotokana na matokeo na mitihani yake ya uwakili kuendeshwa mubashara yamepangwa kuamuliwa Oktoba 24 baada ya hoja zake kusikilizwa.

Barunguza alifungua kesi hiyo Mahakama Kuu Masjala Kuu dhidi ya LST, mkuu wa shule hiyo, Dk Benhajj Masoud na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akipinga uamuzi wa chuo hicho kutupilia mbali rufaa yake.

Katika rufaa hiyo, Barunguza anapinga matokeo ya mitihani yake ya muhula wa kwanza na wa pili ya mwaka wa masomo 2019/20 kuonyesha hakufaulu hata baada ya kuyarudia.

Baada ya kufungua kesi hiyo, Barunguza alimwandikia barua jaji kiongozi kuomba aridhie kesi yake kuendeshwa mubashara kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na akaelekezwa kuliwasilisha suala hilo kwa jopo la majaji wanaolisikiliza shauri hilo.

Juma alisema kesi hiyo ina maslahi kwa umma kutokana na kuwa ya Kikatiba inayogusa taasisi ya umma ambayo wadau wakuu ni wananchi pia ikiwa mubashara itawapa fursa wazazi wake walioko mkoani kuisikiliza pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wanaoishi Afrika Kusini, Marekani, Sweden na Lebanon.

Pia alisema Katiba Ibara ya 18 inatoa haki ya kutoa na kupata taarifa ya mambo yanayohusu jamii juu ya masuala mbalimbali. Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Stanley Kalokola alipinga akisema hajaona sababu akihoji kuwa gharama hizo zitabebwa na nani iwapo ombi litatekelezwa lakini Barunguza alisema yeye atazibeba iwapo wataalamu wa Tehama wa mahakama watashindwa kufanikisha.

Chanzo: mwanachidigital