Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inatarajiwa wiki ijayo kutoa uamuzi ikiwa mkazi wa wilayani Kaliua aitwaye Kassim Daudi anastahili kupewa dhamana ama la kutokana na makosa 30 yanayomkabili ya usafirishaji watoto 30 kisha kuwatumikisha shambani kinyume cha sheria.
Mshtakiwa huyo Kassim Daudi anadaiwa kutenda makosa hayo ya kuwasafirisha watoto 30 kutoka nje na ndani ya Mkoa wa Tabora kati ya mwaka 2023 hadi Januari 2024 ambapo awali alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora ambayo kisheria haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa hati ya dharura kwa madai kwamba mshtakiwa amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ya magonjwa ya moyo kwa muda mrefu.