Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Serengeti yaeleza ugumu kuendesha kesi za ukatili

Ukatili Pic Data Mahakama Serengeti yaeleza ugumu kuendesha kesi za ukatili

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Serengeti, Felix Ginene amebainisha hayo leo Jumatatu Desemba 12, 2021 katika kongamano la siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia akisema Mahakama inapata tabu kufikia uamzi kwa kesi hizo kwa kuwa mashahidi hawafiki mahakamani.

"Kuna tatizo kubwa sana hapa ambalo linasababishwa na mila na desturi, wanakatazwa na kutishiwa kutengwa, hivyo inapofikia ukomo wa kesi mahakamani tunazifuta” amesema Ginene.

Amesema matatizo hayo yako kwenye kesi za ukeketaji na zile za vipigo ambazo masuala yanajadiliwa huko kwenye jamii na kwa kuwa zinawahusu zaidi wanawake na watoto ambao wanaonekana kuwa wanyonge kwenye jamii.

"Akina mama wanapigwa na kukatwa na inaonekana wazi kuwa ameumizwa mwishowe hawafiki mahakamani kwa sababu nyingi za mila na desturi, na sisi mahamama kazi yetu si kuwatafuta waje, tunaangalia muda wa kusikiliza kesi kisha tunafuta,"amesema.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Vicent Mashinji amesema tatizo hilo kwa Mkoa wa Mara ni sugu hata kwa kesi za ujangili na mauaji hawafiki licha ya kushuhudia kuwepo kwa matendo hayo.

Advertisement "Kuna haja kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua umuhimu wa kutoa ushahidi ili kukomesha matukio kama haya,"amesema Dk Mashinji

Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania, Rhobi Samwel amesema tatizo la ukatili ni kubwa mikakati shirikishi inatakiwa.

"Watoto wa kike wanafanyiwa ukatili sana hasa ukeketaji, tunapowapokea wengi huwawapokei lakini wakishafanikiwa kwa elimu na kazi huwahitaji tena, tushikamane kwa elimu ili kuleta mabadiliko,"amesema.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz