Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kuu yawaachia huru waliodaiwa kuua

67084 Kuua+pic

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania  imewafutia  kesi ya mauaji Musa Malaki na wenzake baada ya Serikali ya Tanzania kutokuwa tayari kuendelea na kesi hiyo.

Mbali na Malaki washtakiwa wengine ni Amon Kwambaza na Joseph Chamageo.

Wakili wa Serikali, Lilian Rwetabura amedai leo Jumanne Julai 16, 2019 kwamba kupitia kifungu cha sheria cha makosa ya jinai (CPA)namba 91, kesi hiyo itafutwa, kutokana upande wa Jamhuri  kutoendelea kusikiliza shtaka hilo.

Rwetabura amedai kutokana na kifungu hicho watuhumiwa watakuwa huru lakini kifuñgu hícho pia kinaruhusu watuhumiwa kukamatwa tena kutokana na kosa hilo.

Kufuatia hatua hiyo upande wa utetezi hawakuwa na pingamizi lolote juu ya uamuzi  wa kufutwa kwa kesi hiyo.

Baada ya maelezo hayo msajili wa mahakama hiyo Pamela Mazengo alifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha sheria cha makosa ya jinai namba 91 kama ilivyoelezwa na upande wa Jamhuri lakini washtakiwa watakamatwa tena kwa shtaka hilo.

Pia Soma

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa  kuwa Julai 8, 2015 maeneo ya Msasani wilaya ya Kinondoni, wanadaiwa kumuua Charles Makange.

Chanzo: mwananchi.co.tz