Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kuu yaamuru wadaiwa Exim wakamatwe

Mahakama Pc Dataggg Mahakama Kuu yaamuru wadaiwa Exim wakamatwe

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) jijini Dar es Salaam,imeagiza kukamatwa kwa wadeni watatu wa Benki ya Exim Tanzania kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa deni lenye thamani ya Sh674.4 milioni na zaidi ya Dola 2 milioni za Marekani.

Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa kwa wadeni hao iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi ya kibiashara nambari 95 ya mwaka 2015, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, ameagizwa na Mahakamana kuwakamata wadeni hao watatu ambao ni Chimanbhai Marghabai Patel, Pratik Chimanbhai Patel na Sonia Pratik Patel.

Hata hivyo, Kamanda Masejo alipozungumza na Mwananchi jana alisema hana taarifa juu ya hilo.

Kwa mujibu wa hati hiyo iliyosainiwa Septemba 13, 2021 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, inasema watatu hao walihukumiwa Septemba 16, 2016 kuilipa

Benki ya Exim Tanzania Limited hata hivyo mpaka sasa fedha hizo hazijalipwa kwa benki hiyo.

Hivyo, imeelezwa kuwa kutokana na ucheleweshaji huo wa malipo, Mahakama imeamuru watu hao wakamatwe na wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo. Advertisement

“Unaagizwa kurudisha hati hii mnamo tarehe 27 Oktoba, 2021, sambamba na uthibitisho unao onyesha siku na namna ambavyo hati hii imetekelezwa au sababu zilizosababisha kushindwa kutekelezwa kwake,” inasomeka sehemu ya hati hiyo.

Chanzo: mwananchidigital