Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahabusu wanne kati ya 16 waliotoroka Mbagala wakamatwa

Mahabusu Pc Data Mahabusu wanne kati ya 16 waliotoroka Mbagala wakamatwa

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kati ya mahabusu 16 waliotoroka kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai, Mbagala wilayani Temeke, wanne tayari wamekamatwa.

Septemba 4, mwaka huu Mwananchi liliripoti kutoroka kwa watuhumiwa hao waliokuwa wamehifadhiwa katika kituo hicho baada ya kumpiga askari kisha kuvunja mlango wa chumba cha mahabusu na kukimbia.

Akizungumza Septemba 8, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema jeshi hilo linaendelea kuwasaka waliosalia na kuongeza kuwa lazima watakamatwa wote.

“Nasema hivi, hadi sasa mahabusu wanne wameshapatikana, tunaendelea kuwatafuta wengine 12 ambao hawana sehemu ya kukimbilia, wote watakamatwa tu,” alisema Kamanda Muliro.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita saa 1:30 usiku katika kituo hicho.

Mwananchi ilifika kituoni hapo na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara na wakazi wanaoishi karibu na kituo hicho ambao walikiri kutokea kwa tukio hilo.

Mfanyabiashara Said Abdallah alidai kuwa akiwa katika shughuli zake alisikia kelele za mahabusu waliokuwamo ndani ya kituo cha polisi.

Amesema waliposogolea karibu waliona kundi la watu likiruka uzio wa seng’enge uliozunguka kituo hicho na kutokomea.

“Wakati wakitoroka ndipo askari walianza kupiga risasi hewani mara nne mfululizo, hali ilikuwa tete. Unavyoona eneo hili watu waliacha biashara zao na kukimbia ili kunusuru maisha na mmoja wa watuhumiwa alipita hapa na kuvuka barabara kuelekea ng’ambo ya pili,” alidai shuhu

Chanzo: Mwananchi