Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maduka matano yaporwa milioni 21/- Kibiti

512f4adb08028d625acdcc83645e2d42 Maduka matano yaporwa milioni 21/- Kibiti

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MADUKA makubwa matano likiwemo la wakala wa fedha katika mji mdogo wa Mjawa Magharibi wilayani Kibiti mkoani Pwani yamevunjwa na kuporwa Sh milioni 21.

Taarifa zilizopatikana eneo la tukio zilisema Sh milioni 21 zimechukuliwa na majambazi hao.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya kipolisi ya Rufiji, Onesmo Lyanga uvamizi huo ulifanyika saa 8:00 usiku wa kuamkia juzi.

Kamanda alisema uvunjaji huo ulibainika asubuhi wakati watu wanaenda katika shughuli.

Mmoja wa wafanyabiashara waliovunjiwa na majambazi hao, Shaaban Matandiko alisema amerejeshwa nyuma na kuviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza waliohusika.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mjawa Magharibi, Mohamed Jongo alisema hilo ni tukio la pili kufanyika kijijini hapo. La kwanza lilikuwa la majambazi kumkatakata sehemu za mwili mwananchi kwa kutumia mapanga.

Alisema serikali ya kijiji hicho imeshawasiliana na vyombo vya dola ili vipeleke wataalamu kubaini wahusika na kwenye duka la fedha la M-Pesa jumla ya Sh milioni nne ziliibwa.

Kamanda Onesmo alisema watu kadhaa wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo wakiwamo walinzi wa maduka hayo.

“Siwezi kuzungumzia lolote kuhusu tukio hilo, maofisa wa jeshi hilo wapo katika uchunguzi ...tuna uhakika tutawanasa na watafikishwa kwenye vyombo vya serikali,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz