Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madereva wavunja sheria kukiona cha moto    

Aebdd73cf39bf68596721b475c389975.jpeg Madereva wavunja sheria kukiona cha moto    

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa jeshi hilo halitomvumilia dereva yeyote atakayevunja sheria za usalama barabarani na wamepanga kuendesha operesheni za mara kwa mara ili kuwabaini madereva wa aina hiyo.

Mutafungwa amesema hayo alipokuwa katika operesheni ya utoaji elimu kwa madereva wa mabasi Katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Nchi ipo katika amani hivyo asitokee mtu akasababisha watu wengine wasiwe na amani kwa kusababisha ajali zinazotokana na uzembe” amesema Mutafungwa.

Chanzo: habarileo.co.tz