Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madanguro marufuku "Polisi washughulikieni"

Screenshot 2021 11 01 At 09.png Madanguro marufuku

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa, ameyataja maeneo yanayotumika kwa ajili ya biashara ya udanguro maarufu kama Madada Poa ambapo ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha biashara hiyo kwenye maeneo hayo inakoma mara moja.

Agizo hilo amelitoa kwenye kikao cha cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Tanga, Mgandilwa ameyataja maeneo yenye madanguro kuwa ni eneo la Sabasaba na Barabara ya Uhuru na kusema kuwa wanaofanya biashara ya kuuza mwili kwenye maeneo hayo watafute miji mingine.

"Kuna maeneo kwetu sisi bado kuna madanguro ambayo Dada zetu wanajiuza naomba nitumie hadhara hii kwakuwa vyombo vya dola vipo hapa niwaombe tuanze kushughulika na hawa Watu natamani tuone mji wetu unakuwa safi hatutaki kuona hizi biashara za kujiuza jeshi la polisi wakati mkifanya operesheni zenu basi mshughulike na Watu hawa" DC Mgandilwa.

Katika hatua nyingine Mgandilwa amesema pamoja na hayo analipongeza jiji hilo kwa kuweza kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi na kutaka kuwalipa fidia wananchi ambao bado wana migogoro ya fidia zao lengo ni kuondokana na migogoro isiyokuwa na lazima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live