Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari wafunguka 'ishu' ya Bima kwa Wote

Bimapiic Data Madaktari wafunguka 'ishu' ya Bima kwa Wote

Wed, 18 Jan 2023 Chanzo: Habarileo

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema mchakato wa bima ya afya kwa wote ni kuunga mkono mapendekezo ya shirika la afya Duniani (WHO) na kusema kuwa wanauga mkono asilimia 100 mchakato wake.

Akizungumza na Dar Es Salaam, Rais wa MAT, Dk. Deusdedit Ndilanha pia alitoa mapendekezo ambayo yanatakiwa kuzingatiwa na Serikali.

Ndilanha amesema Muswada wa bima ya afya kwa wote ni mzuri Kwasababu utakuwa na chombo cha kuratibu na kusimamia mfuko huo na yale majukumu ya NHIF kuwa kama polisi,mahakama wamepunguziwa na wao wanajua mzigo wao ulikuwa mkubwa.

"Jambo lingine tunaloona ya kuwa muswada huu ni muhimu ni hatua tuliyochukua ni muhimu sana kwa mujibu wa shirika la afya Duniani ukitaka kuiimarisha huduma za afya unatakiwa kuwa na mambo sita na nguzo kuu ni kugharamia huduma za afya na hizo zingine zinakuwa zimeimarika na tunaona serikali sasa inatekeleza kwa vitendo mapendekezo ya WHO,"ameeleza.

Ndilanha amesema lingine ni uzoefu ambao wameupata kama watoa huduma ikilinganisha mapato kabla ya bima ya afya na baada ya bima ya afya utofauti umeonekana kwamba wameweza kujiendesha kwa watu wachache waliojiunga wameleta mapinduzi ambapo asilimia 15 ikitolewa na kwenda kwenye 50 huduma zitaboreshwa zaidi.

Chanzo: Habarileo