Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Macho na masikio kwa Mbowe, Kisutu leo

FREEMAN AIKAEL Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,Freeman Mbowe

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Freeman Mbowe anatarajia kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Jijini Dar es Salaam leo Agosti 6,kusomewa mashitaka yanayomkabili ya Ugaidi na kupanga njama za mauaji ya Viongozi.

Mbowe anatarajiwa kuwasili Mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi, kwa mujibu wa maelezo ya Wakili wake Peter Kibatala.

Mbowe atafikishwa mahakamani leo baada ya siku ya Jana Agosti 5, kesi yake iliyopangwa kusikilizwa kwa njia ya mtandao kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona, kushindwa kusikilizwa kutokana na hitilafu za kimtandao hivyo Hakimu Mkazi Thomas Simba kuahirisha kesi hiyo na kuagiza afikishwe mahakamani hapo hii leo.

Mbowe na wenzake kadhaa walikamatwa julai 21,mwaka huu Jijini Mwanza walipokwenda kuhudhuria Kongamano la kushinikiza Katiba Mpya.Hata hivyo wenzake waliachiliwa na Mbowe akafikishwa mahakamani kwa Mara ya Kwanza Julai 26,akishitakiwa kwa makosa ya Ugaidi na Kupanga njama za Mauaji ya Viongozi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live