Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maaskari Tanapa washikiliwa polisi kuwajeruhi wananchi watano

Hukumu Pc Data Maaskari Tanapa washikiliwa polisi kuwajeruhi wananchi watano

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia askari watatu wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa) wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa madai ya kuhusika na tukio la kuwashambulia wananchi kwa kipigo na kupora ng'ombe 200 na kujeruhi watu watano wakiwepo wanawake watatu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Mei 12, 2023 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Christian Musyani amesema kukamatwa kwa askari hao ni kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera alililotoa jana Mei 11, 2023 baada ya kufànya ziara katika Kijiji cha Mwanavala kujua undani wa tukio hilo.

“Mpaka sasa tunawashikilia watu watatu ambao ni askari wa Tanapa katika tukio hilo watu watano walijeruhiwa wakiwepo wanawake watatu na wanaume wawili ambao hali zao zinaendelea vizuri,”amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera Mei 11,2023 alilazimika kufanya ziara katika kijiji hicho kuzungumza na wananchi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa maelekezo kwa watendaji wa Serikali wenye dhamana katika sekta ya Maliasili na Shirika la Hifadhi la Taifa (Tanapa) na uongozi wa Mkoa wa Wilaya kutatua mgogoro wa wananchi na hifadhi hiyo.

“Nimeamuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga kuhakikisha askari wote waliohusika katika tukio hilo wanabainika, kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwani Serikali haijawatuma kufanya kitendo hicho cha kinyama kwa wananchi,”amesema.

Hatua ya agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilitokana na Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Francis Mtega kutoa hoja ya dharura jana bungeni Dodoma kutaka kusitisha shughuli zake na kuzungumzia mgogoro wananchi na hifadhi uliotokea Mei 6 mwaka huu na kusababisha wananchi zaidi ya watano kujeruhi na mifugo 200 kuporwa, huku mbuzi na mbwa wakiuwawa kwa kupigwa risasi.

Mtega alilieleza kuwa katika tukio hilo wanawake walivuliwa nguo na kuunguzwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao kitendo ambacho amekieleza kuwa ni cha fedheha kwa wananchi jimboni kwake na kuleta uchonganishi baina ya Serikali na wananchi.

Kufuatilia kauli hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali tayari ilitoa mwongozo baada ya kufanya ziara Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya kwa maelekezo kuwa vijiji 27 havitoweza kuondolewa kutokana na maeneo hayo kutokuwa na tija kwa uhifadhi kwa sasa.

Mkazi wa Mswisi, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya Mathias Shija amesema kuwa Serikali inapaswa kuangalia namna bora ya kuwaondoa wafugaji na siyo kutumia nguvu kubwa ya kupiga wananchi, kuwajeruhi na kuwadhalilisha wanawake kwa kuwavua nguo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live