Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi ya aliyekua Mkurugenzi wa NIDA na wenzake

MAIMU DicksonMaimu na Wenzake

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemkuta na kesi ya kujibu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na wenzake wanne na hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea, Agosti 25 na 26, mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili uamuzi kama washtakiwa wanakesi ya kujibu au laa.

Maimu na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka 55 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 1.175.

Wakati wa usikilizaji wa uamuzi Hakimu mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu amesema amepitia mashtaka yote na vielelezo vyote, na kuridhika kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu na hivyo wanatakiwa kujitetea.

Washtakiwa hao wamedai kuwa watajitetea kwa kiapo na watakuwa na mashahidi pamoja na vielelezo.

Hakimu Chaungu baada ya kueleza hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 25 na 26, 2021 watakapoanza kujitetea washtakiwa hao.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya, amedai mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya uamuzi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Ntalima, Avelin Momburi, Xavery Silverius na Mkurugenzi wa sheria NIDA, Sabina Raymon

Chanzo: www.tanzaniaweb.live