Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maafisa watumia gari la Mkuu wa Mkoa kufanya uhalifu, wadakwa

Pingu 1140x640 Maafisa watumia gari la Mkuu wa Mkoa kufanya uhalifu, wadakwa

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Jamii

Maafisa watatu wa Ushirika wanadaiwa kutumia gari la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kufanya uhalifu katika Ofisi za Vyama vya Kilimo na Masoko (AMCOS) na kukusanya Tsh. Milioni 2.5 katika ofisi 2, waliposhtukiwa wakakimbia na kutelekeza gari Bariadi.

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge kuhusiana na tuhuma hizi, ambaye amesema;

“Ni tukio la kweli, mtuhumiwa Mustafa Kimomwe anashikiliwa, wawili wamekimbia na wanaendelea kutafutwa, madai kuwa walikuwa na bastola hilo tumeambiwa lakini hatujui kama ni ya kweli au bandia kwa kuwa hatujaiona.”

Chanzo: Jamii