Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maadili yatajwa chanzo cha mauaji nchini

Mauaji KMNJRO Maadili chanzo cha mauaji mengi

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuporomoka kwa maadili, tamaa ya fedha na mali pamoja na visasi vimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia vitendo vya kikatili yakiwamo mauaji yanayoripotiwa kila kukicha.

Hayo yalibainishwa juzi na Askofu mstaafu wa Kanisa la Assemblies Of God Jimbo la Kilimanjaro, Glorious Shoo alipozungumzia kukithiri kwa matukio ya mauaji nchini

“Mauaji yanayoendelea kutokea nchini yanaonyesha tuko nyakati za mwisho katika kipindi ambacho fedha imeanza kuonekana ni ya muhimu kuliko utu,” alisema Shoo ambaye ni mchungaji kiongozi wa Kanisa la Kimataifa la Kilimanjaro Christian Church (KICC).

Aliongeza kuwa “jambo lingine linalochangia haya ni mmomonyoko wa maadili kuwa mkubwa. Utagundua hali ya watu kukutana halipo siku hizi kutokana na kukua kwa utandawazi.”

Aliwakumbusha viongozi wenzake wa dini kuwa wana wajibu wa kuhimiza toba, mshikamano na upendo miongoni mwa wanajamii kupunguza matukio hayo.

“Viongozi wa dini tuna kazi kubwa ya kufanya, kwanza kabisa ni kuomba toba mbele za Mungu, damu inayomwagika ya watu ni nyingi hivyo tunapaswa kuhubiri upendo na mshikamano katikati ya jamii ili kupunguza matukio haya yanayogharimu maisha ya wengi,” alisema.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live