Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MPYA: Hakimu amaliza kupitia uchambuzi wa mashahidi kesi ya kina Mbowe

98581 Hukumu Kinambowe+pic MPYA: Hakimu amaliza kupitia uchambuzi wa mashahidi kesi ya kina Mbowe

Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba amemaliza kupitia na kuchambua ushahidi uliotolewa na mashahidi nane wa upande wa mashtaka na mashahidi 15 wa upande wa utetezi . Kinachofuata kwa sasa ni kupitia baadhi ya kesi zinazofanana na kesi hiyo pamoja na kutafsiri sheria. Tofauti na hukumu nyingi zinazotolewa mahakamani hapo, leo ulinzi umeimalishwa hata kwa hakimu anayesikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi hao wa Chadema. Leo askari watatu wamesimama nyuma ya hakimu Simba, mmoja yupo katikati, mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa Lushoto.

Endelea kutufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi.

Chanzo: mwananchi.co.tz