Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MCL yafafanua taarifa za aliyekuwa mfanyakazi wake kuhusika na dawa za kulevya

70738 Pic+july

Sat, 10 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd imesema Julieth Kulangwa, anayedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya nchini Italia si mfanyakazi wake tena na kampuni haihusiki kwa lolote na tukio hilo.

Taarifa ya kampuni hiyo ilisema kuwa Kulangwa alifukuzwa kazi kwa sababu ya kutoonekana kazini kwa zaidi ya siku tano bila taarifa, na hivyo si mfanyakazi wa MCL tangu Julai 8, 2019.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Mwananchi, Francis Nanai, muda anaodaiwa kukamatwa Kulangwa alikuwa kwenye safari zake za binafsi ambazo kampuni ya MCL haihusiki nazo kwa kuwa alikuwa likizo.

“Kulangwa alikuwa likizo na hatuingilii shughuli za wafanyakazi wetu wanapokuwa likizo. Tunaweza kusema ni tukio la kusikitisha kwake yeye na kwa familia yake kujikuta katika mazingira hayo ya aibu,” alisema Nanai.

Alisema MCL haifumbii macho matukio ya usafirishaji wa dawa za kulevya, matumizi na biashara zake na hivyo itatatoa ushirikiano kwa mamlaka zinazohusika katika shauri hilo.

“Hizi ni taarifa za kuvunja moyo zinazohusisha mtu ambaye alikuwa mfanyakazi wetu. Alikuwa Italia kwa sababu zake, si kwa majukumu ya MCL na hivyo kampuni haihusiki kwa lolote na mambo yake binafsi,” alifafanua.

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz