Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAUAJI: Mtoto auawa, kisa kupendwa

64904 Pic+majai

Mon, 1 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtoto huyo inaelezwa aliuawa na kaka kutokana na kupendwa na wazazi

Beldina Nyakeke, Mwananchi [email protected]

Tarime. Mniko Chacha (20) mkazi wa kijiji cha Getenga wilayani hapa mkoani Mara, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mdogo wake, Hassan (7) kutokana na wivu kuwa alikuwa akipendwa na wazazi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe aliiambia Mwananchi kwa n simu jana kuwa tukio hilo lilitokea Juni 26 wakati mtuhumiwa na Hassan walipokuwa machungani.

Mwaibambe alisema mtuhumiwa anadaiwa kumpiga kwa fimbo mdogo wake kabla ya kuanza kumnin’giniza kichwa chini miguu juu huku akimwachia na kuanguka chini.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini majeraha sehemu mbalimbali za mwili wa marehemu ambaye kabla ya kifo alikuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Kitugutiti.

Pia Soma

Kamanda huyo alisema miongoni mwa upendeleo uliomchukiza mtuhumiwa hadi kumshambulia na kusababisha kifo cha mdogo wake, ni kitendo cha baba yao kumwita Hassan jikoni mara kwa mara huku yeye hafanyiwi hivyo.

Alisema baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka wakati wasamaria wema walipokuwa wameelekeza akili na juhudi zao kuokoa maisha ya Hassan.

Katika tukio lingine, Mwaibambe alisema wamewatia mbaroni na kuwafikisha mahakamani raia watatu wa China kwa tuhuma za kusafirisha gramu 300 ya mawe yenye aina mbalimbali za madini kinyume cha sheria.

Alisema walikamatwa katika barabara ya Tarime-Sirari eneo la Nkende Tarime wakisafirisha mawe hayo kwa gari aina ya Toyota Land Cruiser.

Chanzo: mwananchi.co.tz