Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAUAJI: Achinjwa katika mazingira ya kutatanisha

85795 Pic+mauaji MAUAJI: Achinjwa katika mazingira ya kutatanisha

Mon, 25 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mkazi wa Arusha, Sirili John amepatikana ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.

John ambaye alikuwa mfanyabiashara wa matunda katika eneo la Friends Kona jijini Arusha mwili wake ulipatikana juzi.

Akizungumza na Mwananchi, Noel Peter ambaye ni jirani wa marehemu alisema walipata taarifa jana kuhusu kupatikana mwili wa Paul maarufu kama rasta akiwa amechinjwa. “Hatujui kilichotokea ila tumepata taarifa amekutwa amechinjwa na watu wasiojulikana lakini polisi wanachunguza” alisema.

John pia inadaiwa alikuwa mgombea wa Chadema nafasi ya ujumbe wa mtaa wa mnara wa Vodacom, katika kata ya Unga Ltd jijini Arusha kabla ya chama hicho kujitoa.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Raphael Peter alisema kuna utata wa kifo hicho kwani kuna taarifa zikihusisha na ugomvi wa mapenzi.

“Kuna mengi yanazungumzwa wengine wanasema mambo ya mapenzi wengine ni siasa lakini ukweli utajulikana” alisema

Mhudumu wa chumba cha kuhifadhi miili katika hospitali ya mkoa Mount Meru, Francis Costa alithibitisha kupokelewa mwili wa John

“Mwili uliletwa hapa na leo (jana ) umechukuliwa na kupelekwa Katesh kwa mazishi na alikuwa amechinjwa,” alisema

Hata hivyo, Costa alisema vyombo vya dola vinafuatilia tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo.

Hata hivyo, ofisa mmoja wa polisi ambaye aliomba kuhifadhiwa jina alisema taarifa za awali za kifo hicho zinahusishwa na mambo ya mapenzi.

“Wanachunguza zaidi lakini nilichosikia kwa baadhi ya watu mambo ya mapenzi yanatajwa,” alisema.

John anatarajiwa kuzikwa leo Katesh wilayani Hanang mkoa wa Manyara.

Chanzo: mwananchi.co.tz