Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KUADHIMISHWA KESHO

359fb3e4c2b18c45a5ca1137823d5429 MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KUADHIMISHWA KESHO

Thu, 10 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAADHIMISHO ya siku ya Kimataifa ya Kupambana na Rushwa na Siku ya Kimataifa ya haki za Binadamu yatafanyika jijini Dodoma kesho.

Kaulimbiu ya maadhimisho kwa mwaka huu ni 'Uzingatiaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa Viognozi na Watumishi kwa Ustawi wa Utawala Bora na Haki za Binadamu nchini'

Maadhimisho ya mwaka huu yatashirikisha wadau wa sekta ya umma na sekta binafasi, taasisi zizizo za kiserikali pamoja na wabia wa maendeleo .

“ Tumejipanga kukumbushana juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya ahadi ya uadilifu ambao ndio mwongozo wa mwenendo wa watumishi waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi katika sekta ya umma na binafasi,” amesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika.

Chanzo: habarileo.co.tz