Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAHAKAMANI: Ilivyokuwa Kesi ya kujiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli Nyumbani

Fri, 23 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Mfanyakazi Mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (TAZAMA) Samwel Nyakirang’ani (63) na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kujiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iwapatie dhamana.

Maombi hayo wameyawasilishwa kupitia Wakili wao, Kusalika Augustine mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo alidai wateja wake wanahitaji kupata dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.

Kutokana na maombi hayo, upande wa mashtaka uliomba kesi hiyo iahirishwe ili wajibu hoja hizo, ambapo Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi February 22, 2018.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Nyangi Mataro ambaye ni Mwalimu wa Shule ya  msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

Wengine ni mfanyabaishara, Farijia Ahmed, Malaki Mathia, Kristomsi Angelus, Pamfili Nkoronko na Hunry Fredrick.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali Bomba la Mafuta ya  Dizeli, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.

DPP kutoa uamuzi kuhusu Mhasibu wa TAKUKURU



Ilivyokuwa katika kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Tembo



 
Chanzo: millardayo.com