Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lita 232 za dizeli ya treni zawaingiza matatani

51486 Pic+mafuta

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewakamata wakazi wawili wa Nzega kwa tuhuma za kukutwa na lita 232 za dizeli kutoka kwenye treni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Aprili 10, 2019, kamanda wa polisi mkoani Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea juzi katika eneo la Ugusule, wilayani Nzega.

Amesema walipata taarifa saa kumi jioni kuwa watu wana mafuta ya wizi mali ya Shirika la Reli nchini.

Amesema walipofuatilia waliwakamata Sabuni Omary na Doto Kahogo, waliokutwa na dizeli lita 232 mali ya Shirika la Reli.

Amesema mafuta hayo yalikuwa katika madumu kumi na mbili, kati ya madumu hayo kila moja lilikuwa na lita ishirini na moja lita 12.

Kamanda Nley pia amesema wanamshikilia dereva wa treni, Hamza Hamis, kwa tuhuma za kufuja mafuta ya dizeli yaliyokuwa kwenye treni yake.

Amesema wanamhoji dereva kuhusiana na mafuta hayo na wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo.

Mkazi wa mtaa wa Kiyungi, kata ya Kitete, Simon Bahati amesema ni vizuri Shirika la Reli likadhibiti mali zake kwa vile zinahujumiwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz