Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leo ni Birthday ya Neymar na Ronaldo, fahamu rekodi zao

2652 Skysports Neymar Ronaldo Real Madrid 4149369 660x400

Tue, 6 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Neymar wa Paris Saint Germain ya Ufaransa leo February 5 wote wawili wanasherehekea Birthday zao, Neymar na Ronaldo wote wamezaliwa mwezi mmoja na tarehe kama ya leo.

Ronaldo leo anasherehea kutimiza umri wa miaka 33 wakati Neymar yeye anasherehekea kutimiza umri wa miaka 26, kila mmoja anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani japo Neymar inaaminika huu sio utawala wake atatamba sana baada ya Ronaldo na Messi.



Cristiano Ronaldo anatimiza umri wa miaka 33 akiwa mafanikio ya kushinda Ballon d’Or mara tano, kiatu cha dhahabu Ulaya mara nne, tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya mara tatu, Mchezaji bora wa FIFA wa kiume mara mbili na tuzo ya mchezaji bora wa Dunia.

Kwa upande wa Neymar akiwa na umri wa miaka 26 bado hajafanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or wala ya FIFA lakini anapewa nafasi ya kuwa katika list ya wachezaji wanaotarajiwa kuja kushinda tuzo hizo baada ya utawala wa Messi na Ronaldo kumalizika.

VIDEO: John Bocco na Mzamiru Yassin walivyoifungia Simba leo vs Ruvu Shooting

Chanzo: millardayo.com