Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema atakiwa kuripoti polisi Machi 24

98092 Lema2+pic Lema atakiwa kuripoti polisi Machi 24

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Jeshi la Polisi mkoani Singida limemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na kumtaka kuripoti tena Machi 24 mwaka huu. Lema anatuhumiwa kusambaza taarifa za mauaji ya watu 14 Wilaya ya Manyoni mkoani hapa na kulilaumu jeshi hilo kuwa halijachukua hatua zozote jambo ambalo si kweli. Kauli hiyo anadaiwa kuitoa wakati akizungumza katika mazishi ya Katibu wa Chadema Jimbo la Singida Mashariki, Alex Joas aliyeuawa kwa kitu chenye nja kali wilayani Manyoni mkoani Singida. Machi 2 mwaka huu Lema alikamatwa na polisi jijini Arusha na kisha kusafirishwa usiku huo hadi mkoani Singida. Akizungumza leo Alhamisi Machi 5 mwaka huu mara baada ya kuachiwa huru, Lema amesema kukamatwa kwake hakumtishi kwa sababu anatimiza wajibu wake. Amesema ataendelea kupaza sauti sehemu yoyote atakayobaini kuwa kuna tatizo kama hilo na kwamba hata katika mkutano wa Bunge unaoanza mwishoni mwa mwezi huu pia atalizungumzia. Wakili wa Lema, Hemed Nkulungu ameliomba Jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo kwa sababu mteja wake ana majukumu mengi ya kitaifa. Amesema kila raia ana haki ya kutoa taarifa ya makosa ya uvunjifu wa sheria kama Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inavyotamka.

Chanzo: mwananchi.co.tz