Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lauwo aondolewa mashtaka kesi ya kina Hans Poppe, Aveva

23040 POP+PIC TanzaniaWeb

Sat, 20 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeondoa mashtaka ya mfanyabiashara Franklin Lauwo katika  kesi inayowakabili viongozi wa klabu ya Simba, akiwamo mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zachalia Hans Pope.

Hata hivyo, anaendelea kutafutwa na akipatikana ataunganishwa na wenzake.

Uamuzi huo  umetolewa leo Ijumaa Oktoba 19,2018  na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka kushindwa kupata Lauwo.

Lauwo anakabiliwa na shtaka la kuendesha shughuli za ukandarasi bila kuwa na leseni kupitia kampuni yake ya Ranky  ambayo haijasajiliwa na bodi ya makandarasi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro akisaidiana na Mutalemwa Kishenyi amedai kuwa Lauwo bado hajajisalimisha katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

"Lauwo alikuwa ajisalimishe leo  Takukuru, lakini mpaka sasa ameshindwa kufanya hivyo na nimewasiliana na wenzetu wa Takukuru asubuhi hii (leo)  wameniambia bado hajajisalimisha,” amesema Kimaro.

"Hivyo chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, tunaomba Mahakama yako kumuondoa katika hati ya mashtaka ili kesi iweze kuendelea."

Kimaro baada ya kueleza hayo,  Hakimu Simba aliondoa shtaka hilo.

"Mahakama imeondoa mashtaka ya Lauwo  kama walivyoomba upande wa mashtaka,  hivyo kupitia kifungu hicho Mahakama itawasomea maelezo ya awali  washtakiwa watatu ambao wapo mahakamani hapa,” amesema Hakimu Simba.

Mbali na Hans Pope, viongozi wengine wa simba katika kesi hiyo ni rais wa Simba, Evans Aveva  na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili ni  matumizi mabaya ya madaraka kwa kuhamisha fedha za klabu bila idhini ya kamati ya utendaji ya simba, kughushi,  kuwasilisha nyaraka za uwongo na mashtaka ya utakatishaji fedha yanayowakabili Aveva na Kaburu.

Mashtaka ya Hans Poppe yazua mvutano mahakamani

Endelea kufuatilia MCL Digital kwa taarifa zaidi za kesi hiyo

Chanzo: mwananchi.co.tz