Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Laki 8 yamtupa jela miaka 20

HUKUMU miaka 20 jela kwa wizi wa simu

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Wilaya ya Temeke leo Jumatano Agosti 4, imemuhukumu mkazi wa Mtongani jijini Dar es Salaam, Joakim Komba maarufu Domo la Mbwa au Pilato (21) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kuiba kiasi cha Sh, 880,000 na simu yenye thamani ya Sh. 350,000.

Pia mahakama hiyo imeamuru mshtakiwa huyo kuchapwa viboko 10 kabla ya kuanza kutumikia kifungo hicho.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Jimson Mwankenja akisema mahakama hiyo imezingatia adhabu iliyoanishwa katika kifungu cha 227A ya kanuni ya adhabu unyang'anyi wa kutumia silaha haitakiwi kuwa chini ya miaka 30 jela.

Chanzo: Mwananchi