Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Laana ya bibi yampeleka miaka 30 jela

87334 Pic+jela Laana ya bibi yampeleka miaka 30 jela

Fri, 6 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Misungwi. Mahakama ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imemhukumu mkazi wa kijiji cha Nange, Shabo Marando (47) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka bibi.

Hakimu Esther Malick alitoa adhabu hiyo baada ya kuridhika pasi na shaka na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa mashataka akiwamo Dk Judith Kiwango wa hospitali ya wilaya hiyo aliyemfanyia uchunguzi na kumkuta na michubuko na manii sehemu za siri.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Esther alisema ameridhika na ushahidi huo, hivyo anamhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo hicho ili liwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Alipotakiwa kujitetea kabla ya kupewa adhabu, mshtakiwa alidai mlalamikaji ni shemeji yake na kukana kumbaka bali alimpa eneo la kulima na siku ya tukio alikamatwa na wananchi baada ya kuchota maji ya kumwagia nyanya zake katika dimbwi lililokuwa limekatazwa kutumiwa.

Awali, mwendesha mashtaka wa polisi, Juma Kiparo alidai Julai 9 kitongoji cha Igokelo, mshtakiwa akifahamu ni kosa alimbaka mwanamke huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz