Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LISSU: Kufuta kesi ya Mbowe sio kuingilia uhuru wa Mahakama

Tundu Lissuww Tundu Lissu

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema suala alilomuomba Rais Samia la kufuta kesi ya Mbowe sio kuingilia Uhuru wa Mahakama, wanaweza kufanya kama walivyofuta kesi ya Masheikh wa Uamsho.

Amesema hayo katika mahojiano na Kituo cha VOA akifafanua hajamwambia Rais aongee na Jaji bali Mwendesha Mashtaka ambaye ni mteule wa Rais na anafanya kazi kama sehemu ya Serikali Kuu na sio sehemu ya Mahakama.

Tangu Mh.Tundu Lissu akutane na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan kuliibuka sintofahamu ya hoja ambazo Lissu aliamua kuzitaja kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kile alichozungumza na Rais Suluhu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live